Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amesema kuwa msingi wa sera za CCM utabakia kuwa ni maendeleo ya watu pamoja na amani na utulivu wa nchi.
Balozi Nchimbi aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na mamia ya wananchi wa mji wa Songea katika maeneo ya Liziboni, Uwanja wa Majimaji na Mshangano, ambapo wananchi walikusanyika kwa hamasa kubwa kumsikiliza licha ya kuwa kwenye ziara nyingine za kikazi.
Katika eneo la Liziboni, Balozi Nchimbi alilazimika kusimamisha msafara wake ili kuzungumza na wananchi waliomsimamisha njiani akitokea Nyasa. Alitumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi wa Songea kwa mchango wao mkubwa uliomuwezesha kufahamika kitaifa na kimataifa.
Katika Uwanja wa Majimaji, alihutubia umati mkubwa wa wananchi waliokuwa wakimsubiri wakati alipofika kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la ghorofa lenye fremu 50 za CCM Mkoa wa Ruvuma.
Katika hotuba yake, aliwaomba wananchi wa Songea, mkoa mzima na nchi nzima kwa ujumla kujiandaa kushiriki kwa wingi Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, 2025.
Akiwa Mshangano, Balozi Nchimbi alizindua rasmi fremu 50 za tawi la CCM la eneo hilo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.