• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MSOMI wa shahada aliyenufaika na TASAF atoa ushuhuda wake kwenye maonesho ya Kilimo nanenane Mbeya

Imewekwa kuanzia tarehe: August 8th, 2023

Mnufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF ambaye ni msomi shahada ya kwanza  ya masuala ya maendeleo ya jamii Lightness Mwasano ambaye ni mkazi wa Kata ya Kalobe mtaa wa Majengo jijini Mbeya akisuka mkeka katika banda la TASAF kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF umeendelea kuwasaidia watoto waliozaliwa katika kaya masikini kufikia ndoto zao.

Hayo yameelezwa na Lightness Mwasano Mkazi wa Kata ya Kalobe mtaa wa Majengo jijini Mbeya ambaye ni mmoja wa wanufaika wa mfuko wa TASAF na mshiriki wa maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane kupitia banda la TASAF  amesema kupitia mfuko huo umemsaidia kusoma shule mpaka kufikia ngazi shahada ya kwanza masuala ya Maendeleo ya jamii katika  chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).

Amesema baba yake alifariki mwaka 2009 na mama kubaki mjane ambapo alikua na watoto watatu huku akiwa Hana kazi na aliwalea kwa kuuza mbogamboga.

Amesema mama yake alishindwa kumudu ghalama za kuwalea na kupata mahitaji muhimu ikiwemo ya shule kutokana na kutokuwa na kipato cha kuendesha maisha katika familia.

“Mama alienda kujieleza Kwa viongozi wa serikali ya mtaa hivyo walimshauri kujiunga na mfuko wa TASAF na kweli tulisaidiwa kusoma mpaka nilipomaliza elimu yangu ya sekondari  kidato cha nne wakati nipo kidato cha tano mkoani Kigoma  mama aliugua na kufariki”amesema Lightness

Amesema baada ya mama yake naye kufariki bado TASAF waliendelea kuwahudumia katika maswala mbalimbali yakiwemo ya kielimu na kijamii.

Aidha Lightness ameongeza kuwa ameweza kusoma mpaka kufikia chuo kikuu kwakuwa alipata  mkopo wa asilimia 100 ambao pia uliwasaidia wadogo zake kwenye mahitaji yao ya Kila siku shuleni na nyumbani.

Amesema kupitia TASAF hata Sasa mdogo wake ambae yupo kidato Cha sita anaendelea kunufaika na mfuko huo huku akiamini ataweza kusoma na kupatiwa mkopo wa serikali kwa asilimia 100.

Hata hivyo amepongeza juhudi zinazofanywa na serikali chini ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kusaidia wanyonge huku akitoa wito kwa kaya zisizoweza kujikimu na kusaidia watoto wao kupata elimu kwenda kujieleza kwenye serikali za mitaa ili waweze kuingizwa kwenye mfuko huo na kupata msaada na kutimiza ndoto zao





Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.