• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MTATIRO aagiza mfumo wa stakabadhi ghalani kusimamiwa kikamilifu

Imewekwa kuanzia tarehe: August 4th, 2023

MKUU wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma MheshimwaJulius Mtatiro,amewaagiza viongozi wa vyama vya msingi vya Ushirika(Amcos)na idara ya Ushirika Halmashauri ya wilaya Tunduru kuhakikisha wanadhibiti utoroshaji wa zao la mbaazi na kuimarisha mfumo wa stakabadhi ghalani ili kuwasaidia wakulima waweze kujiinua kiuchumi.

Mtatiro amesema hayo , wakati akizungumza na mameneja na wenyeviti wa Amcos,maafisa tarafa na viongozi wa Chama kikuu cha Ushirika(Tamcu katika kikao cha maandalizi ya makusanyo ya zao  hilo na mazao mchanganyiko kwa msimu wa masoko 2023/2024.

“Mwaka jana kulikuwa na ucheleweshaji kutokana na watu wa mifumo kuchelewa kufanya uzembe  hali iliyopelekea kuchelewa kuanza msimu wa makusanyo na ununuzi wa mbaazi,mwaka huu sitaki kusikia hali hiyo inajitokeza tena”alisema.

Aidha alisema,zao mbaazi katika msimu  2023/2024 litaendelea kuuzwa kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani na kuwaonya wakulima,viongozi,watunza maghala na wanunuzi wanaokusudia kuharibu mfumo huo ambao umeonyesha mafanikio makubwa kwa wakulima.

Amewataka viongozi wa vyama na bodi za Ushirika  wilayani humo,kuwa waaminifu na kuepuka kujihusisha na ubadhirifu,bali wahakikishe wanaongoza vyama hivyo kwa kufuata taratibu na sheria za vyama vya Ushirika.

“hakutakuwa na huruma kwa yoyote atakayejaribu kuvuruga ununuzi wa mbaazi katika msimu wa mwaka huu,nawaombeni sana viongozi wenzangu  twendeni tukawasaidia wakulima wetu huko  vijijini”alisisitiza Mtatiro.

Amewataka wakulima,kutokubali kudanganywa na wafanyabiashara wanaopita kwenye maeneo yao kwa ajili ya kuhitaji kununua mbaazi  nje ya mfumo huo  kwa bei ndogo isiyolingana na gharama za uzalishaji na kueleza kuwa,serikali imejipanga kuwashughulikia watu hao.

Alisema,mfumo wa soko huria ni  wa kinyonyaji na hauna nafasi tena katika wilaya hiyo kwa kuwa ndiyo uliosababisha wakulima wa mikoa ya kusini kuendelea kuwa maskini kwa muda mrefu licha ya jitihada kubwa wanazofanya mwaka hadi mwaka.

Alisema,dhamira ya serikali ni kuona sekta ya kilimo inawanufaisha wakulima kwa kupata fedha  zinazostahili na serikali inapata ushuru ambao utakwenda kutumika kuharakisha maendeleo na kuboresha huduma muhimu za kijamii.

Mtatiro,amewaasa viongozi na watendaji wa sekta ya ushirika kuhakikisha wanakutana na wakulima  ili kuwaeleza faida za ushirika na maafisa ugani kuwatembelea kwenye shughuli zao mara kwa mara ili kuwapa ushauri wa kilimo cha kisasa na chenye tija kwa kuwa wakulima wakisimamiwa vizuri watazalisha kwa wingi na AMCOS  zitapiga hatua kubwa ya kiuchumi.

Afisa ushirika wa wilaya hiyo George Bisan alisema,msimu wa mwaka 2020/2021 na 2021/2022 changamoto kubwa ilikuwa utoroshaji wa zao la mbaazi kwenye vijiji vinavyopakana na  mikoa jirani ambayo hakuwa mfumo huo.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa TAMCU Iman Kalembo  alieleza kuwa, katika msimu 2022/2023 Chama kikuu kwa kushirikiana na vyama vya Ushirika vya msingi viliweka malengo ya kukusanya kilo milioni 5,451,000.

Hata hivyo alisema kuwa,kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao walifanikiwa kukusanya kilo milioni 3,035,692 ambazo ni pungufu kwa kilo milioni 2,415,308  sawa na anguko la asilimia 44.31 ya lengo.

Kalembo alieleza kuwa,mbaazi ziliuzwa kwa kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani na jumla ya minada sita ya mauzo ilifanyika ambapo bei  ya wastani ilikuwa Sh. 898.25 na  jumla ya kilo 3,035,692 ziliuzwa zenye thamani ya Sh.bilioni 2,633,233,690.00.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBUNGE Kawawa aleta neema Namtumbo

    May 11, 2025
  • KIONGOZI Mwenge wa uhuru ashiriki upandaji miti Songea

    May 11, 2025
  • MWENGE wa uhuru waweka jiwe la msingi shule ya amali Songea

    May 11, 2025
  • MWENGE wa uhuru wazindua jengo la EMD Peramiho

    May 10, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.