Ukitaka kushuhudia maajabu ya asili, historia ya ukombozi wa Afrika, na uzuri wa utalii wa kipekee unaovutia kwa macho na roho, basi safari yako lazima ipitie Mto Ruvuma ,mto mrefu kuliko yote Afrika Mashariki na kati.
Mto Ruvuma ni mto ambao haupokei sifa kwa ukubwa wake pekee, ukiwa na urefu wa zaidi ya kilomita 800 na upana wa hadi mita 720 .
Chanzo Kidogo, ukubwa wa kushangaza
Kama simulizi ya hadithi za kale, chanzo cha Mto Ruvuma kipo katika milima ya Matogoro, Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Kisima kidogo tu kilicho meta 1500 kutoka usawa wa bahari. Lakini kutoka hapo, mfereji huo mdogo huanza safari ya kuandika historia katika wilaya zote tano za Mkoa wa Ruvuma: Songea, Mbinga, Nyasa, Namtumbo na Tunduru.
Mto wa Uzima na Maendeleo
Mto Ruvuma si mto tu wa kupendezesha mandhari; ni moyo unaodunda kwa jamii na viumbe hai kusini
Fukwe, Visiwa na Wanyama Pori
Kuelekea wilaya ya Namtumbo na Tunduru, Mto Ruvuma hubadilika kuwa mto wa ndoto kwa watalii.
Hifadhi ya mazingira asilia ya Mwambesi inatoa mandhari ya kipekee ,visiwa vidogo, fukwe nzuri, na safari za mitumbwi.
Hapa, tembo, simba, swala, mamba, na samaki wa aina mbalimbali hutawala kando mwa Mto Ruvuma wakivutia watalii kutoka ndani na nje ya nchi.
Katika Pori la Akiba la Liparamba wilayani Nyasa, maporomoko ya Nakatuta ni kivutio kingine. Wageni huja kuvua samaki, kupiga picha, na kupanda miamba ya asili iliyobeba historia ya miaka mingi.
Historia Iliyogubikwa na Maajabu
Mto Ruvuma haujaishia kwenye uzuri wa kiasili pekee; ni shahidi wa harakati za uhuru. Katika eneo la Mwambesi, maji haya yalitumika katika Vita ya Majimaji (1905–1907), na maporomoko ya Sunda yalitumika kama “darubini ya vita ya porini” ya Golira War iliyopiganwa Msumbiji.
Katika eneo hili, ndege mdogo zaidi duniani pantiole huogelea na kuwinda samaki hai, tukio adimu la kihistoria na kibaiolojia.
Mto Ruvuma Unaounganisha Mataifa
Safari ya Mto Ruvuma inaendelea katika daraja la Umoja, mpakani mwa Tanzania na Msumbiji, wilayani Nanyumbu. Daraja hilo lenye urefu wa zaidi ya meta 700 linaunganisha mataifa mawili na siyo kwa daraja pekee, bali kwa urithi wa pamoja wa historia, utalii na amani.
Bahari ya Hindi: Hitimisho la Safari
Mwisho wa safari ya Mto Ruvuma ni katika Bahari ya Hindi, eneo la Msimbati, Mtwara. Hapa, maji ya mto huingia katika Hifadhi ya Bahari ya Ghuba ya Mnazi na Maingilio ya Mto Ruvuma
Hakuna shaka Mto Ruvuma si tu kivutio, bali ni chemchemi ya uhai kwa Watanzania na majirani zao wa Msumbiji.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.