Mtoto Baraka Nicolaus Mbunda (12) mwenye ulemavu wa viungo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma amekabidhiwa amekabidhiwa vifaa vitakavyomsaidia kutokana na changamoto alizonazo.
Baraka ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Huruma amekabidhiwa vifaa kiti mwendo na vifaa vingine na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mheshimiwa Desderius Haule alifanya ziara katika shule hiyo kwa lengo la kujionea hali halisi ya changamoto zinazomkabili mwanafunzi huyo.
Licha ya kukabidhi kiti mwendo Mwenyekiti huyo wa Halmashauri pia alimkabidhi mwanafunzi huyo kiti maalum kitakamchosaidia mwanafunzi huyo wakati wa kupata haja kubwa na ndogo ikiwa ni hatua za awali zilizochukuliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga katika kumpunguzia adha na changamoto mtoto huyo kutokana na hali ya ulemavu aliyonayo.
Akizungumza baada ya kukabidhi vifaa hivyo Haule amebainisha kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga itaendelea kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya mtoto Baraka na kwamba kuna jitihada mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa ili kuwafikia watoto wengi zaidi wenye mahitaji maalum katika Halmashauri hiyo.
“Halmashauri itafanya kila kitakachowezekana kuhakikisha mtoto Baraka anasoma na kufikia ndoto zake pia Halmashauri inajenga shule ya Watoto wenye mahitaji maalum katika Kata ya Maguu ili kuhakikisha Watoto wenye ulemavu wanapata fursa ya kupata elimu’’.alisisitiza Haule.
Mwenyekiti huyo pia ametoa wito kwa wazazi na na jamii kwa ujumla kutowaficha watoto wenye ulemavu na kwamba wanatakiwa kuthaminiwa na kupewa haki ya kupata elimu kama watoto wengine.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.