Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe. Kapenjama Ndile amewataka viongozi kutoa ushirikiano kwa mwekezaji wa Bustani ya Manispaa Songea Hamza Mohamedy “ DELIGHT GARDEN PARK” ambayo imefunguliwa na kuanza kutoa huduma.
Amewataka wananchi, na wadau mbalimbali kuwekeza katika maeneo ya ndani ya Songea ili kuleta maendeleo ya kiuchumi, uwekezaji, viwanda na fursa za kitalii.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Komredi Oddo Mwisho ametoa wito kwa Waheshimiwa Madiwani kuendelea kushirikiana na wataalamu na kuhamasisha wadau waweze kuja kuwekeza katika Maeneo mbalimbali ili kuleta maendeleo kwa wananchi wa Manispaa ya Songea.
Mwekezaji huyo ametumia shilingi milioni 348 kuwekeza katika bustani hiyo inayotarajia pia kutoa ajira kwa vijana,
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.