MRADI wa Chuo cha Ufundi Stadi (Veta) wenye thamani ya zaidi Bilioni 2 umekataliwa kuwekwa Jiwe la Msingi na Kiongozi wa Mbio za Mwenge maalumu wa Uhuru Kitaifa Lt. Josephine Mwambashi kutokana na mapungufu yaliyobainika.
Akikagua mradi huo Mwambashi amebaini mapungufu ni pamoja na matumizi makubwa ya rasilimali fedha kuliko uhalisia wa majengo husika chuoni hapo mfano kibanda cha mlinzi kujengwa kwa gharama ya shilingi milioni 15 Jambo alioliona ni ufujaji wa fedha za Umma.
“Nakuagiza TAKUKURU kuanza kufanya uchunguzi wa kina juu ya gharama halisi zilizotumika kujenga mradi huo kuanzia sasa”.
Wakati huohuo katika kuwawezesha wananchi kiuchumi Kiongozi huyo alipata fursa ya kukagua na kuzindua shamba darasa la Michikichi lenye ukubwa wa hekari 5.8 ambalo limegharimu jumla ya zaidi ya shilingi milioni 6.
Mwambashi amepongeza juhudi za Halmashauri kwa kuhamasisha vijana kujiunga na vikundi ili kuhamasisha wakulima wengine kuendeleza zao hili ili kuongeza kipato na kuleta tija kwa jamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Nyasa akiwasilisha taarifa kwa kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwamba kuanzisha kwa shamba darasa hili ni kutoa elimu kwa wakulima ili waweze kulima zao la chikichi na kuzalisha mafuta na kuongeza kipato kwa wananchi na Serikali kwa ujumla, sambamba na kutekeleza uhaba wa mafuta ya kula nchini.
Imeandalwa na Aneth Ndonde
Kutoka Ofisi ya Habari Mkoa wa Ruvuma
Septemba 5,2021
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.