Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 Ndugu Abdalla Shaib Kaim ameridhia kufungua mradi wa kuboresha huduma ya maji safi katika kata za Bethlehem ,Matarawe na Ruhuwiko Halmashauri ya mji wa Mbinga mkoani Ruvuma unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.5
Akitoa taarifa kwa Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa mazingira Mbinga (MBIUWASA ) amesema mradi huo ulikamilika Machi 2022 na kuongeza idadi ya watu wanaopata maji katika mji wa Mbinga kutoka zaidi 39,000 hadi watu zaidi ya 51,000.
Kiongozi Wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 Ndugu Abdalla Shaib Kaim amewapongeza MBIUWASA kwa kutekeleza mradi huo katika viwango vinavyokubalika na kulingana na thamani ya fedha.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.