MBIO maalum za Mwenge wa Uhuru zinatarajia kuanza mkoani Ruvuma Septemba mbili na kukamilika Septemba saba mwaka huu.Kwa mujibu wa ratiba ya Mwenge wa Uhuru kitaifa 2021,Mwenge unatarajiwa kupokelewa katika kijiji cha Sautimoja wilayani Tunduru ukitokea mkoani Mtwara Septemba mbili ambao utakimbizwa wilayani Tunduru.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo Septemba tatu, Mwenge wa Uhuru utakimbizwa wilaya ya Namtumbo,Septemba nne Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika Halmashauri mbili za wilaya ya Mbinga,Septemba tano utakimbizwa katika wilaya ya Nyasa na Septemba sita Mwenge wa unatarajia kuhitimisha mbio zake katika Halmashauri tatu za wilaya ya Songea ambazo ni Halmashauri ya Songea,Manispaa ya Songea na Halmashauri ya Madaba.
Jumla ya miradi 41 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni kumi inatarajiwa kupitiwa na Mwenge wa Uhuru mwaka huu ambapo Septemba saba mwaka huu Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kukabidhiwa mkoani Njombe
Kaulimbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka huu ni
"TEHAMA ni msingi wa Taifa endelevu,itumie kwa usahihi na uwajibikaji"
"Kupambana na rushwa ni jukumu langu"
"Mshikamano wa kitaifa, tuwajibike kwa pamoja"
"Tujenge jamii yenye afya imara kuzingatia lishe bora"
"Ziro malaria inaanza na mimi,nachukua kuitokomeza"
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.