• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MWENGE wa Uhuru ulivyowamwagia sifa viongozi Tunduru

Imewekwa kuanzia tarehe: April 20th, 2023

KIONGOZI wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa 2023 Abdalla Shaib Kaim,ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa jitihada zake za kuimarisha na kuboresha sekta ya afya hapa nchini.

Kaim ametoa pongezi hizo jana,wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la huduma za dharura katika Hospitali ya wilaya Tunduru mkoani Ruvuma.

Alisema tangu serikali ya awamu ya sita iingie madarakani miaka miwili iliyopita, imeonyesha kwa vitendo dhamira ya kuwatumikia Watanzania hususani wananchi wa kawaida kwa kuwaondolea changamoto mbalimbali zilizokuwepo kwa muda mrefu ikiwemo huduma bora za afya.

Alisema, lengo la serikali kujenga jengo hilo ni kuhakikisha hakuna mwananchi anaweza kupoteza maisha kwa kukosa huduma za matibabu na kutoa wito kwa wakazi wa wilaya ya Tunduru kuwa  na mazoea  ya kwenda na kutumia vituo vya kutolea huduma vilivyopo katika maeneo yao kwa ajili ya kupata matibabu.

Amewaagiza vongozi wa wilayaya Tunduru,kukamilisha  ujenzi wa jengo hilo haraka ili wananchi waanze kupata huduma na kufaidi matunda ya Serikali yao badala ya kuchukua muda mrefu.

“haya ni matunda yanayofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan,katika kuimarisha sekta ya afya hapa nchini”alisema Kaim.

Aidha,amemwagiza Mganga Mkuu wa wilaya hiyo kutoa mafunzo kwa watumishi watakaofanya  kazi katika jengo hilo ili wawe na ujuzi zaidi wa kutumia vifaa vitakavyofungwa na namna ya kuwahudumia wagonjwa watakaoletwa kupata matibabu.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya Tunduru Dkt Athuman Mkonoumo alisema,ujenzi wa jengo hilo unatekelezwa kwa gharama ya Sh.milioni 369,683,004.10 kati ya hizo Sh.milioni 300 zimetolewa na Serikali huku Sh.milioni 69,683,004.10 ni mapato ya ndani ya Halmashauri.

Alisema,jengo hilo linajengwa kwa mfumo wa Force Akaunti na ujenzi wake ulianza rasmi mwezi Februari na ulitarajiwa kukamilika mwezi Mei mwaka jana,lakini kutokana na changamoto mbalimbali mradi haukuweza kukamilika kwa muda uliopangwa.

Dkt Mkonoumo alisema, kwa sasa ujenzi umefikia asilimia 98 na kazi zilizosalia ni ukamilishaji wa ufungaji wa viyoyozi, na uwekezaji wa mfumo wa hewa tiba utakaowekwa na wataalam kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi.

Alieleza kuwa,kukamilika kwa mradi huo kutasaidia sana utekelezaji wa azma ya Serikali ya kutoa huduma bora za afya kwa wananchi wake hasa ikizingatiwa kuwa wilaya ya Tunduru ni kubwa kwa eneo na ina idadi ya watu wapatao 412,054.

Alisema,mradi huo utawezesha kupunguza rufaa za matibabu kwa wagonjwa na kupunguza gharama za matibabu kwa wananchi wanaostahili kupata rufaa kwenda Hospitali nyingine nje ya wilaya ya Tunduru.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.