• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MWENGE wa Uhuru wafungua na kuweka mawe ya msingi miradi ya bilioni 1.45 Tunduru

Imewekwa kuanzia tarehe: April 17th, 2023

MWENGE wa Uhuru umeanza mbio zake mkoani Ruvuma kwa kukagua na kuweka mawe ya msingi katika miradi yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.448 wilayani Tunduru.

Miradi iliyowekewa mawe ya msingi ni  ujenzi wa mradi wa maji safi na salama katika Kijiji cha Muhuwesi ambao hadi sasa umegharimu zaidi ya shilingi milioni 175 na mradi wa jengo la dharura(EMD)  katika hospitali ya wilaya ya Tunduru  ambao hadi sasa umetumia zaidi ya shilingi milioni  334.

Miradi mingine ni mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa ya TEHAMA na samani zake unaogharimu zaidi ya shilingi milioni 899 na mradi wa madarasa mawili katika shule ya msingi Nandembo wenye thamani ya shilingi milioni 40.

Akitoa taarifa ya mradi wa maji Muhuwesi kwa kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023,Meneja wa RUWASA wilaya ya Tunduru Mhandisi Maua Mgallah  amesema mradi huo ulioanza kutekelezwa Mei 26,2022 unatarajia kukamilika Aprili 30,2023.

Amesema utekelezaji wa mradi huo hadi sasa umefikia zaidi ya asilimia 90 na kwamba utakapokamilika kwa asilimia 100 utahudumia wakazi wapatao 7494 waliopo katika Kijiji cha Muhuwesi.

Kwa upande wake Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru Chiza Marando akitoa taarifa ya mradi wa jengo la dharura EMD katika hospitali ya wilaya ya Tunduru,amesema mradi ulianza kutekelezwa Februari 25,2022 na kwamba hadi sasa umefikia asilimia 95 na kwamba unatarajia kukamilika Aprili 30,2023.

“Kukamilika kwa mradi huu kutasaidia azma ya serikali  ya kutoa huduma bora  za afya kwa wananchi wake na kwamba Tunduru ina barabara kuu ya Mtwara korido  kwa kuwa kuna wagonjwa  wengi wa kawaida na wanaopata ajali wataweza kupata huduma hivyo kupunguza rufaa  za matibabu kwa wagonjwa’’,alisisitiza Marando.

Akizungumza kwa nyakati tofauti wakati anaweka mawe ya msingi kwenye miradi hiyo ,Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Abdalah Shaib Kaim ameupongeza uongozi wa wilaya ya Mbinga kwa usimamizi mzuri wa miradi.

Hata hivyo Shaib ameagiza miradi yote kukamilika kwa asilimia 100 kama ilivyoelezwa kwenye taarifa ili wananchi waanze kunufaika na miradi hiyo ambayo serikali imetoa fedha nyingi za kuhakikisha miradi inatekelezwa na kumaliza kero kwa wananchi.

Katika hatua nyingine kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa amefungua miradi ya ujenzi wa vyumba  viwili vya madarasa vyenye thamani ya shilingi milioni 40 katika shule ya msingi Nandembo na mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa ya TEHAMA na samani zake vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 899 katika sekondari ya Kiuma.

Mwenge wa Uhuru umeanza mbio zake mkoani Ruvuma kuanzia Aprili 17,2023 na unatarajia kukamilisha mbio hizo Aprili 25,2023 ambapo utakabidhiwa katika Mkoa wa Njombe.

Akizungumza kwenye makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru kati ya  Mkoa wa Lindi na Ruvuma,Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Stephen Ndaki amesema ukiwa mkoani Ruvuma Mwenge wa uhuru utatembelea miradi 61 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 16.

Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

Aprili 17,2023,Tunduru 

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.