Kiongizi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 Ndugu Abdalah Shaib Kaim amegawa vyandarua kwa akinamama na watoto chini wa mienzi 9 Halmashauri wa Wilaya Tunduru mkoani Ruvuma
Zoezi hilo limefanyika leo Aprili 17, 2023 katika Shule ya Msingi Nakapanya wilayani umo mara baada ya makabidhiano ya kimkoa baina ya Mkoa wa Lindi na Ruvuma ya Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2023 yaliofanyika katika kijiji cha Sauti moja wilayani Tunduru.
Kaim amesema Mwenge wa Uhuru unatambua juhudi zinazofanya na Serikali kupitia Wizara ya Afya pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo juu ya kupambana ugonjwa wa Malaria sambamba na mpango wa Taifa wa kudhibiti Malaria wa (NMCP)
“Niwaambie watanzania wezangu mjenga nchi ni mwananchi mwenyewe tuhakikishe tunavitumia vyandarua hivi kama tulivyopewa maelekezo na wataalamu wa Afya ili kujinginga na mbu aenezae ugonjwa wa Malaria huo ndio wito wangu”alisema Kaim.
Hata hivyo amewasisitiza Wananchi kuacha tabia ya kuvitumia vyandarua hivyo kinyume na utaratibu ambao unafahamika na kuacha kutumia kwenye shughuli za kilimo cha mboga mboga na katika shughuli ya uvuvi halamu kwa kufanya hivyo ni waaminifu pindi wakipewa vyandarua hivyo
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.