• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MWENGE wa Uhuru wahitimisha mbio zake Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: June 15th, 2024

Mwenge wa Uhuru 2024 umehitimisha mbio zake mkoani Ruvuma kwa kukagua miradi katika Halmashauri ya Madaba wilayani Songea.

Akitoa taarifa kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa 2024 kuhusu mradi wa ujenzi wa maji katika Kijiji cha Mbangamawe Halmashauri ya Madaba,Meneja wa RUWASA Wilaya ya Songea Mhandisi Mathias Charles  amesema RUWASA ilipokea Zaidi ya shilingi milioni 545 kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji katika Kijiji hicho.

Amesema utekelezaji wa mradi huo umehusisha ujenzi wa tanki lenye uja zo wa lita 50,000,ujenzi wa banio la maji,ujenzi wa sampu tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 30,000,nyumba ya  mtambo,chumba cha mlinzi,choo na vituo sita vya kuchotea maji .

Amesema mradi huo una faida mbalimbali zikiwemo  wananchi wapatao 2,800 kunufaika na upatikanaji wa huduma  ya maji na salama hivyo kupunguza umbali wa kufuata maji.

Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Halmashauri ya Madaba umeweka jiwe la msingi ujenzi  mradi wa  lami nyepesi barabara ya Kifaguro-Magingo  yenye urefu wa kilometa 5.6

Mradi huo unatekelezwa na TARURA kwa gharama ya Zaidi ya shilingi milioni 563 ambapo kukamilika kwa ujenzi wa mradi huo,kutarahisisha wananchi wa Halmashauri hiyo kufika kwa urahisi katika jengo la Makao makuu ya Halmashauri, hospitali ya Wilaya,shule ya msingi Kifaguro na sekondari ya Madaba hivyo kupata huduma za kijamii kwa urahisi.

Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Halmashauri ya Madaba pia umekagua mradi wa upandaji miti  katika uhifadhi na utunzaji wa vyanzo vya maji hifadhi ya Wino ambayo ina ukubwa wa  hekta 39,718,Msitu huo unaoundwa na safu tatu za Wino,Ifinga na Mkongotema.

Hifadhi ya Msitu wa Wino inaendelea na uhifadhi wa mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji na kuvitumia katika shughuli za uzalishaji wa miche ya kupanda  na matumizi ya majumbani.

Miongoni mwa vyanzo vya maji muhimu vinavyoendelea kulindwa ni Igawisenga, Mgombezi, Mwendesi na Kibanditi ambapo wananchi wamepanda miti 20,000 itakayosaidia kutunza vyanzo vya maji,kuimarisha kilimo cha zao la nyuki na kupanda matunda mbalimbali.

Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Madaba umeweka jiwe la msingi la ujenzi wa soko la Lituta linalogharimu Zaidi ya shilingi milioni 190 na kwamba kukamilika kwa mradi huo kutaongeza mapato katika Kijiji na kuboreshwa mazingira rafiki kwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Godfrey Mnzava amekagua na kuzindua vyumba viwili vya madarasa na matundu matatu ya vyoo katika shule ya msingi Ngadinda ambapo jumla ya shilingi milioni 53 zimetumika kutekeleza mradi huo.

Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Halmashauri ya Madaba ulisomewa taarifa ya ugawaji wa vyandarua kwa akinamama wajawazito na Watoto chini ya mwaka mmoja ambapo katika kipindi cha Julai 2023 had Mei 2024 Halmashauri  hiyo ilipokea vyandarua 5040 vyenye thamani ya  Zaidi ya shilingi milioni 36

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.