Mbio za Mwenge wa Uhuru zimeanza rasmi leo Mei 9, 2025, mkoani Ruvuma kwa kutembelea, kukagua na kuweka mawe ya msingi katika miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
Mwenge wa Uhuru umezindua vyumba viwili vya madarasa ya awali na matundu sita ya vyoo katika Shule ya Msingi Mkwera, umeweka mawe ya msingi katika ujenzi wa nyumba ya wageni katika Kijiji cha Lituta na mradi wa maji kijiji cha Gumbiro na kukagua mradi wa lishe katika Kijiji cha Lutukira.
Akiweka jiwe la msingi katika mradi wa maji katika kijiji cha Gumbiro, Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Bw. Ismail Ali Ussi, amehimiza mamlaka husika kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati ili wananchi wanufaike na juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita na kuwasihi wananchi kutunza miradi hiyo.
Kwa upande wake Mbunge wa Madaba, Mhe. Joseph Mhagama, amesema jimbo hilo katika kipindi cha uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia limepokea bilioni 12.9 kwa ajili ya miradi ya maji.
Ameeleza kuwa mradi huo wa Gumbiro ni moja kati ya miradi ambayo inatarajiwa kukamilika hivi karibuni na mradi huo utakuwa na uwezo wa kubeba maji lita 75,000 na kuhudumia wakazi zaidi ya 2,000.
Mwenge wa Uhuru pia umekagua shughuli za kiuchumi zinazofanywa na vijana wa bodaboda katika Kijiji cha Mbangamawe na kuweka jiwe la msingi katika kituo cha kulelea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu cha Hope Village na kushiriki katika upandaji wa miti ili kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa utunzaji wa mazingira.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.