MWENGE wa Uhuru umeendelea na mbio zake mkoani Ruvuma kwa kupitia miradi nane yenye thamani ya shilingi bilioni 2.1 katika Halmashauri ya Mji Mbinga.
Mwenge wa Uhuru ukiwa mjini Mbinga umekagua mradi wa ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje,jengo la maabara na jengo la upasuaji katika hospitali ya Halmashauri ya Mbinga,mradi ambao unatekelezwa kwa gharama ya Zaidi ya shilingi milioni 900.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo amesema mradi huo ukikamilika utaongeza miundombonu toshelezi kwa watoa huduma na wagonjwa,kupanua wigo kwa watoa huduma za afya kwa makundi maalum na kuanzishwa huduma mpya za kuchunguzi.
Hata hivyo licha ya kuweka jiwe la msingi kwenye mradi huo,Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024 Godfrey Mnzava ameiagiza TAKUKURU kufanya uchunguzi wa kina kwenye mradi huo,baada ya mwenge wa Uhuru kubaini utekelezaji wa mradi huo haukufanyika kupitia mfumo wa manunuzi ya umma wa NeST kama ilivyoelekezwa na serikali.
Mwenge wa Uhuru ukiwa mjini Mbinga umekagua mradi wa kuboresha huduma ya maji safi katika Kijiji cha Utiri na kuweka jiwe la msingi,mradi ambao unagharimu Zaidi ya shilingi milioni 421.
Mradi wa uboreshaji huduma ya maji safi Utiri unahudumia wakazi wapatao 3,857 ambapo lengo la mradi ni kusogeza huduma ya maji ili kuwapunguzia wananchi kero ya kutembea kutafuta maji.
Mradi mwingine ambao umefunguliwa na Mwenge wa Uhuru mjini Mbinga ni ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya msingi Myangayanga ambao umegharimu shilingi milioni 48.
Mwenge wa uhuru umeweka jiwe la kutembelea kiwanda cha kukoboa kahawa Mbinga ,mradi ambao umegharimu Zaidi ya shilingi milioni 725.
Akizungumza kwenye kiwanda hicho,Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Godfrey Mnzava amesema licha ya kiwanda hicho kuwa na manufaa kiuchumi ikiwemo kutoa ajira za kudumu 76 na za muda 300,ameuagiza uongozi kuwanunulia vifaa vya usalama kazini wafanyakazi wote wa kiwanda hicho.
Mwenge wa Uhuru mjini Mbinga umekagua mradi wa shamba la mbegu bora za miti katika Kijiji cha Utiri lenye ukubwa wa ekari 23.8 linalomilikiwa na Halmashauri ya Mji wa Mbinga na kuendeshwa kwa ubia kati ya Halmashauri ya Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kwa ufadhili wa Ubalozi wa Finland.
Mradi huo umegharimu Zaidi ya shilingi milioni 55 na kwamba lengo la mradi ni kuzalisha mbegu bora za miti ambazo zinapatikana kwa urahisi na kwa gharama nafuu.
Mwenge wa Uhuru ukiwa mjini Mbinga pia umepokea taarifa ya mapambano dhidi ya malaria ambapo Halmashauri imenunua vyandarua 43,955 vyenye thamani ya Zaidi ya shilingi milioni 404 ambavyo vimegawiwa bure kwa wajawazito, ,Watoto na wanafunzi ili kufikia adhima ya serikali ya Ziro Malaria ifikapo mwaka 2023.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.