• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MWENGE wa Uhuru waridhia miradi yote Tunduru

Imewekwa kuanzia tarehe: May 16th, 2025

Mwenge wa uhuru umekamilisha ziara yake mkoani Ruvuma kwa kuangazia miradi ya wilaya ya Tunduru ambapo umeweza kuweka jiwe la msingi katika mradi mkubwa wa maji safi na salama  wa Masuguru unaogharimu Zaidi ya shilingi bilioni 2.4.

Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 umezindua , kukagua, kutembelea na kuweka mawe ya msingi katika miradi 11 yenye thamani ya shilingi Bilioni 3.2 wilayani Tunduru 

Meneja wa RUWASA  Wilaya ya Tunduru Mhandisi Maua Mgallah amesema mradi huo uliofikia asilimia  85 ya utekelezaji unakwenda kuwanufaisha wananchi wapatao 16,124 na  kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika wilaya hiyo kutoka asilimia 81.86 hadi kufikia  asilimia 86.65.

Mwenge wa uhuru ukiwa wilayani Tunduru pia umeweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa jengo la kusubiria ndugu wa wagonjwa katika hospitali ya wilaya ya Tunduru ambapo serikali imetenga Zaidi ya shilingi milioni 97 kutoka mapato ya ndani kutekeleza mradi huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Chiza Marando amesema  hadi sasa mradi umefikia asilimia 80 ya utekelezaji na kwamba mradi huo utawawezesha ndugu wa wagonjwa kutoa  huduma mbalimbali kwa wagonjwa na kupunguza msongamano wa ndugu wa wagonjwa katika maeneo ya kutolea huduma hasa  wodini.

Mwenge wa Uhuru ukiwa wilayani Tunduru pia umetembelea shamba la miti katika kijiji cha Chiwana lenye ukubwa wa hekari 8.23  ambalo limepandwa miti hekari 2,3 aina ya mitiki ambalo lina miti 1,551.

Mwenyekiti wa kijiji cha Chiwana Mohamed Chiulika amesema shamba darasa  dogo hilo lilianzishwa mwaka 2021 kupitia mradi wa TASAF lengo likiwa ni kutunza mazingira kupitia upandaji miti.

Amezitaja baadhi ya faida ambazo zimepatikana hadi sasa kutokana na mradi huo ni pamoja na watu 50 kupata elimu ya upandaji miti na utunzaji wa mazingira,miti itakapokomaa kijiji kitaongeza mapato kupitia mbao  na matumizi mbalimbali yanayotokana na miti hiyo yenye soko kubwa kimataifa.

Mwenge wa uhuru ukiwa wilayani Tunduru pia umetembelea mradi wa nishati safi ya kupikia katika shule ya sekondari Tunduru ambao unagharimu Zaidi ya shilingi milioni 24.

Katika sekondari ya Tunduru mwenge wa uhuru pia umepitia mradi wa ujenzi wa mabweni mawili na matundu sita ya vyoo.

Mwenge wa Uhuru ukiwa wilayani Tunduru pia umezindua mradi wa ujenzi w barabara ya nguzo sita-Muungano hadi Camp David yenye urefu wa kilometa 0.5 kwa kiwango cha lami unaotekelezwa na TARURA.

Meneja wa TARURA wilaya ya Tunduru Mhandisi Silnavus Ngonyani  amesema mradi huo umegharimu Zaidi ya shilingi milioni 234.

Mwenge wa uhuru pia umepitia mradi wa ugawaji vyandarua kwa akinamama wajawazito na watoto wa miezi tisa ambapo mradi huo umegharimu Zaidi ya shilingi milioni 59  fedha ambazo zimetolewa na wahisani wa Global Fund.

Mwenge wa uhuru umekagua shughuli za lishe katika Halmashauri hiyo mradi ambao umegharimu shilingi 605,000.

Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Chiza Marando amelitaja lengo la kupunguza na kuzuia tatizo la udumavu katika kipindi cha siku 1000 za mwanzo wa maisha ya mtoto ambapo Halmashauri hiyo imetenga shilingi milioni 70 katika kutekeleza afua za lishe.

Akizungumza kwa nyakati tofauti baada ya kupitia miradi hiyo kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa 2025 Ndugu Ismali Ali Ussi  amewapongeza viongozi wa Halmashauri hiyo kwa kusimamia ipasavyo miradi hiyo ambayo imetekelezwa katika ubora unaolingana na thamani ya fedha.

Ussi amewakumbusha wananchi wote waliojiandikisha  kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba mwaka huu kwenye uchaguzi mkuu  wa Rais,wabunge na madiwani.

Mwenge wa Uhuru umemaliza mbio zake mkoani Ruvuma kwa kupitia miradi katika Halmashauri zote nane ambapo Mei 17 unakabidhiwa katika Mkoa wa Mtwara.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MSIKIMBILIE hasara,serikali inakuja na bei ya neema kwa mahindi Julai

    May 31, 2025
  • WAKULIMA Namtumbo wachuma neema ya ufuta kwa teknlojia mpya ya mnada wa kidigitali

    May 31, 2025
  • RUSHWA yazidi kuporomoka na kukosa nafasi Ruvuma

    May 31, 2025
  • SERIKALI yatoa fidia ya bilioni 2.5 kupisha mradi wa umeme wa Grid Songea-Tunduru

    May 31, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.