Mwenge wa Uhuru umeweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Amali katika kijiji cha Lundusi, Halmashauri ya Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma.
Mradi huo unagharimu shilingi milioni 560.5, ukiwezeshwa na wahisani kupitia Serikali Kuu chini ya mpango wa kuboresha elimu ya sekondari (SEQUIP).
Shule hiyo inalenga kuimarisha sera na mitaala ya elimu ili kuwawezesha wahitimu kupata maarifa na ujuzi wa ujasiriamali, hatua itakayowasaidia kujitegemea na kuchangia maendeleo ya taifa.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Bw. Ismail Ali Ussi, wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi amesema kuwa shule za amali zinajengwa ili wilaya na halmashauri izalishe wataalam wa sekta mbalimbali, kwa lengo la kupunguza utegemezi.
Amesisitiza kuwa Serikali, chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imewekeza fedha nyingi katika miradi mikubwa na ya kimkakati, hivyo wananchi wanapaswa kuunga mkono jitihada hizo na kulinda miundombinu inayojengwa.
Shule hiyo itawezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo katika sekta mbalimbali, zikiwemo viwandani, mashambani, uvuvi, na ujuzi wa kujiajiri au kuajiriwa kulingana na mahitaji ya soko la ajira na mabadiliko ya teknolojia.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.