Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma, Komredi Oddo Mwisho, amefanya ziara ya siku tano Wilayani Tunduru yenye lengo la kuimarisha uhusiano kati ya viongozi na wananchi, kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, na kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo.
Ujumbe wa ziara hii umekuwa ukiongozwa na Komredi Oddo mwenyewe, akiambatana na viongozi wengine wa ngazi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Kamati ya Siasa Mkoa na Wilaya.
Akizungumza katika ziara hiyo kwa nyakati tofauti Komred Mwisho amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na serikali katika kuleta maendeleo huku akiwahimiza kushiriki kikamilifu katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa.
Amesema kuwa uchaguzi huu ni fursa kwa wananchi kuchagua viongozi bora ambao wataweza kuwatumikia kwa uaminifu na kuwaletea maendeleo.
Katika ziara hiyo,Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa alizungumza na wakuu wa Idara na vitengo wa Halmashauri ya Tunduru na wakuu wa Taasisi ambapo aliwataka kutumia ujuzi na utaalamu wao katika kutatua kero za wananchi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.