• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

NAIBU Waziri wa Mazingira atembelea mgodi wa makaa ya mawe Ngaka

Imewekwa kuanzia tarehe: July 21st, 2021

ZAIDI ya wananchi  224 kati yao 100  kutoka katika vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Ruvuma Coal Ltd, unaojihusisha na uchimbaji wa makaa ya mawe katika vijiji vya Ruanda na Sara wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, wamepata ajira  ya kudumu tangu kuanzishwa kwa mgodi huo katika kipindi cha mwaka mmoja.

Meneja wa mgodi huo Benedict Mushingwe amesema hayo, wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa usimamizi na utunzaji mazingira  kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Hamad Chande.

Amesema,kampuni  kupitia mgodi wa Ruvuma Coal Ltd ilifanya uamuzi wa kuchimba madini ya makaa ya mawe ili kuitikia wito wa Serikali wa kuifanya Tanzania kuwa na uchumi wa viwanda kwa kuwa makaa ya mawe ni chanzo cha nishati yenye bei rahisi katika uendeshaji wa mitambo na viwanda.

Amesema, tangu mgodi huo ulipoanzishwa mwaka mmoja uliopita kumekuwa na faida nyingi  zilizopatikana ikiwemo kutoa kandarasi kwa kampuni  nyingine kama vileTNR, Suma Jkt  na Avco ambazo zimechangia kutoa ajira kwa watu 227.

Mushingwe ametaja faida  nyingine zilizopatikana tangu kuanzishwa kwa mgodi huo ni kuchochea ukuaji wa uchumi na biashara kama maduka na vifaa vya ujenzi,mama na baba lishe na huduma za kifedha.

Aidha amesema,mgodi unanunua bidhaa mbalimbali kama nyama,matunda na mboga mboga zinazozalishwa na vijiji vinavyozunguka mgodi kwa ajili ya wafanyakazi wake hali iliyosaidia sana kuchochea kukua kwa uchumi na maisha ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi.

Pia Mgodi wa Ruvuma  Coal Ltd unalipa kodi kwa Mamlaka ya mapato(TRA)malipo ya Mrahaba Tume ya madini,malipo ya tozo kwa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga na kuchangia miradi ya maendeleo ya jamii kwa vijiji vinavyozunguka mgodi.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Hamad Chande amesema, Serikali inapenda  kuwakaribisha wawekezaji kuja nchini kuwekeza kwenye migodi  kwa  maslahi ya wananchi na nchi yetu.

Hata hivyo,amewataka wamiliki wa migodi ya makaa ya mawe kuzingatia sheria na taratibu za uhifadhi wa mazingira katika maeneo wanayochimba, kwa kupanda miti  na yahakikishe yanakuwa na mpango madhubuti kurejesha ardhi katika hali ya awali mara baada ya shughuli ya uchimbaji kukamilika ili kulinda afya za binadamu wanaoishi  kwenye vijiji vinavyozunguka mgodi huo.

Amesema,mazingira ndio uhai wa binadamu,hivyo ni lazima kuyatunza na kuyalinda kwa gharama yoyote na ameagiza magari yote yanayosafirisha makaa ya mawe kudhibiti vumbi kwa kufunga maturubai wakati wa kusafirisha ili lisisambae  hadi kwenye makazi ya watu.

Naibu Waziri Chande,amemuamgiza Mkuu wa wilaya ya Mbinga Aziza Mangosongo  kushirikiana na watendaji wa vijiji na kata kuhakikisha madereva wa malori na  wamiliki wa migodi wanatekeleza sheria za usalama na utekelezaji wa usimamizi na utunzaji wa mazingira.

“uwekezaji wowote ni lazima uzingatie Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004,ikiwa ni pamoja na kufanya tathimini ya athari ya mazingira kwa kuwa ni takwa la kisheria”amesema.

Amewataka wataalam wa Baraza la Taifa la usimamizi wa mazingira(NEMC) kanda ya Kusini, kufanya  ukaguzi wa mara kwa mara kwenye migodi  ili kuhakikisha masuala ya uzingatiaji wa sheria ya mazingira yanakuwa endelevu.

Mkuu wa wilaya ya Mbinga Aziza Mangosongo amesema, zipo changamoto za kimazingira  zinazotokana na shughuli za migodi  kwa baadhi ya  makampuni kutozingatia taratibu za kimazingira kwa kumwaga maji katika maeneo ya mgodi na  barabarani pale yanaposafirisha makaa ya mawe kwenda katika maeneo mbalimbali.

Aidha amemueleza Naibu Waziri Chande  kuwa,kucheleweshwa kwa mchakato wa ulipaji wa fidia  kwenye maeneo ya uchimbaji hasa kampuni ya Ruvuma Coal Ltd ambayo hadi sasa bado haijalipa fidia kwa wananchi  vya Sara na  Ruanda waliochukuliwa maeneo yao kupisha shughuli za uchimbaji kumepelekea kuwepo kwa malalamiko mengi.

Amesema, baadhi ya makampuni  kuhifadhi makaa ya mawe kwa muda mrefu zaidi ya miezi sita bila kuzingatia taratibu za kiusalama na kimazingira, hivyo kuhatarisha usalama wa wananchi wa vijiji vinavyozunguka migodi hiyo.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.