Naibu Waziri wa Nishati Mheshimiwa Judith Kapinga kwa kushirikiana na Kampuni ya Gesi ya Oryx Tanzania amegawa jumla ya majiko ya mitungi ya gesi 850 yenye thamani ya shilingi milioni 76 kwa wananchi wa Wilaya ya Mbinga, Mkoa wa Ruvuma.
Ugawaji wa mitungi hiyo yenye unalenga kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Kupitia Mkakati wa Taifa wa matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia (2024-2034), Serikali imedhamiria kuongeza kaya za watanzania zinazotumia nishati safi ya kupikia kutoka asilimia 10 ya sasa mpaka kufikia asilimia 80 ifikapo mwaka 2034.
Naibu Waziri wa Nishati Mheshimiwa Judith Kapinga amesema mpaka sasa Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), imesambaza mitungi ya gesi ya ruzuku 83,500 yenye thamani ya Shilingi bilioni 3.5 bilioni.
Hata hivyo Naibu Waziri amesema katika mwaka huu wa fedha serikali imepanga kutoa mitungi ya gesi 452,445 yenye thamani ya Shilingi bilioni 10.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.