Rais Samia awezesha gari kufika kwa mara ya kwanza ,wananchi wasema malaika ameshuka
SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imewezesha kwa mara ya kwanza tangu uhuru gari kufika kwenye kijiji cha Ndonga Kata ya Riwundi Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.
Serikali kupitia TARURA imetoa zaidi ya shilingi milioni 200 kutengeneza barabara ambayo haikuwepo tangu nchi kupata uhuru mwaka 1961.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amekagua barabara hiyo ambapo amemshukuru Rais kwa kufungua Mawasiliano ya barabara katika kijiji hicho ambacho kiligeuka kisiwa.
Serikali katika kijiji hicho licha ya kutengeneza barabara,pia imepeleka huduma ya umeme na kujenga zahanati.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.