Miaka michache iliyopita, maji safi yalikuwa ndoto kwa familia nyingi mkoani Ruvuma. Kina mama walitembea kilometa nyingi kila alfajiri na watoto walikosa masomo wakisaka tone la maji. Lakini leo, hali hiyo imegeuka kuwa simulizi ya zamani.
Kwa uwekezaji wa zaidi ya shilingi bilioni 228.92, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kupitia miradi mbalimbali imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya maji—kutoka vijijini hadi mijini, kila kona ya Ruvuma sasa inanufaika na huduma bora za maji safi na salama.
Katika halmashauri zote nane za mkoa wa Ruvuma miradi ya maji imetekelezwa kwa kasi na ubora wa hali ya juu. Kupitia juhudi hizo, wananchi wanafurahia upanuzi wa mtandao wa maji safi uliowafikia maelfu ya wakazi waliokuwa wakikosa huduma hiyo ya msingi kwa miaka mingi. Mitandao mipya ya mabomba, matenki ya kisasa na visima virefu vimejengwa, huku huduma zikifikishwa hadi kwenye taasisi za umma kama shule, vituo vya afya na maeneo ya biashara.
Mji wa Songea, ambao ni kitovu cha maendeleo ya mkoa, umeshuhudia utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji unaogharimu shilingi bilioni 145 unaotegemewa kuwa mkombozi wa kudumu kwa wakazi wake. Mradi huu umejumuisha ujenzi wa miundombinu ya kisasa ya uchujaji na usambazaji wa maji, hatua ambayo imerahisisha upatikanaji wa maji kwa zaidi ya asilimia 90 ya wakazi. A
Sauti za shukrani kutoka kwa wakazi wa Mkoa wa Ruvuma sasa zinasikika kila kona,kutoka kwa wakulima waliopata muda zaidi wa kushughulikia mashamba yao, hadi kwa wanafunzi waliopata fursa ya kuhudhuria masomo bila bughudha ya kutafuta maji.
Hakika, uwekezaji huu si tu umeleta maji, bali umeleta hadhi, afya na matumaini mapya kwa wakazi wa Ruvuma. Ni ushahidi kuwa pale dhamira ya kweli inapowekwa, maendeleo halisi yanawezekana na maji siyo tu uhai, bali ni kichocheo cha mapinduzi ya kijamii na kiuchumi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.