• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

NEEMA yawashukia wakazi 175 wa Songea

Imewekwa kuanzia tarehe: September 18th, 2024

WAKAZI 175 wa mtaa wa Ruhila Seko Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma,wamelipwa Sh.milioni 925.33 kama fidia baada ya kutoa maeneo yao katika bonde la Ruhila ili  kupisha shughuli za uhifadhi wa chanzo cha maji.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Songea(Souwasa) Patrick Kibasa kwa Waziri wa maji Juma Aweso kabla ya hafla ya kukabidhi  hundi kwa wakazi hao.

Alisema,mwaka 2003 Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Songea(Souwasa), ilifanya uthamini kwa wananchi  wa eneo hilo ili waache kufanya shughuli za kibinadamu katika bonde hilo kwa kuwa limekuwa linategemewa kama chanzo kikuu cha upatikanaji wa maji kwa wakazi wa Manispaa ya Songea.

Kibasa alisema,wananchi 803 walifanyiwa uthamini na kuorodheshwa na malipo yao yalifanyika kwa awamu mbili ambapo mwaka 2018 Serikali ilitoa Sh.milioni 500 kwa wananchi 361 waliolipwa fidia.

Kwa mujibu wa Kibasa, mwaka 2019,Serikali ilitoa  Sh.bilioni 1.41 kama fidia kwa wananchi 442 na kukamilisha idadi ya wananchi 803 ambao walikuwepo kwenye orodha ya malipo na baadaye zoezi la uwekezaji wa alama katika eneo hilo lilifanyika.

Hata hivyo Kibasa alisema,wakati wa ulipaji wa fidia ya awamu ya kwanza na pili, wananchi 207 walijitokeza na kulalamika kwamba wameachwa kwenye malipo  na wengine walilalamika kupunywa.

Kibasa alieleza kuwa,kufuatia malalamiko hayo Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Ruvuma iliiagiza Souwasa kushirikiana na Ofisi ya Kamishina wa Ardhi mkoa na Halmashauri ya Manispaa ya Songea kushughulikia malalamiko hayo.

Alisema,baada ya malalamiko hayo kufanyiwa kazi ilibainika wananchi wanaostahili kulipwa ni 175 kati ya 207 na kiasi cha fedha kinachohitajika ni Sh.milioni 925.33.

Katibu Mkuu wa wizara ya maji Mwajuma Waziri,amewashukuru wananchi  hao kwa uvumilivu wao na kusisitiza kuwa,serikali haitegemea kupata malalamiko mengine kutoka kwa wananchi.

Amewataka wananchi  wa Ruhila,kutofanya shughuli zozote za kibinadamu katika eneo hilo,bali wahakikishe wanalinda chanzo hicho kwa manufaa yao na vizazi vingine.

Kwa upande wake Waziri wa maji Juma Aweso alisema,tangu Rais Dkt Samia Suluhu Hassan aingie madarakani miaka mitatu iliyopita amekuwa suluhu ya matatizo ya Watanzania katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Aweso,amewataka watendaji waliopewa dhamana ya kusimamia zoezi la ulipaji fidia,kuhakikisha wananchi hao wanalipwa fedha zao haraka na kutoweka mizengwe kwenye ulipaji wa fidia hizo.

“ Wananchi wamekuwa wavumilivu kwa muda mrefu na fedha hizo ni haki zao,hivyo hakuna sababu za msingi kuchelewesha malipo yao,nawaagiza kuanzia kesho  wananchi wapate fedha kwenye akaunti zao”alisisitiza Waziri Aweso.

Mbunge wa Jimbo la Songea mjini Dkt Damas Ndumbaro alisema,malipo hayo ni ya tatu kufanywa na Serikali  kwa wananchi wa Songea ambapo mara ya kwanza Serikali ilitoa Sh.bilioni 5.700 kwa wananchi waliopisha mradi wa EPZA.

Dkt Ndumbaro alieleza kuwa,mara ya pili  ilitoa Sh. 363 kwa wananchi wa mtaa wa Pambazuko  walipoisha ujenzi wa mradi wa maji  katika eneo hilo,fidia nyingine ni Sh.milioni 400 zililizotolewa kupisha upanuzi wa kiwanja cha ndege  cha Songea,hivyo fedha zilizotolewa kama  malipo kufikia Sh.bilioni 9.600.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa mtaa huo Juma Makweta,amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha zilizofanikisha kulipa fidia wananchi ambao walitoa maeneo yao kupisha  kazi za uhifadhi wa chanzo hicho.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.