Jumla ya walimu 54,000 nchini ambao waliachwa nyuma kimadaraja wanatarajia kupandishwa madaraja yao ifikapo Julai 2024 ili kuleta usawa wa madaraja kwa kuzingatia kiwango cha Elimu na muda wa Ajira.
Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Katibu Mkuu TAMISEMI ambaye pia ni Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma Vicent Kayombo wakati anazungumza na walimu wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma.
“Katibu Mkuu TAMISEMI amenituma nije niwaambie kwanza Serikali inatujali sana sisi walimu haijatusahau inataka walimu wote wawe kwenye hali sawa ikilinganishwa na kiwango cha elimu na madaraja yao’’,alisema Kayombo
Hata hivyo amesema wakati Serikali inaendelea kuboresha sekta ya elimu nchini Kayombo, inawataka walimu hao kutimiza majukumu yao ya kusimamia malezi ya wanafunzi na kuhakikisha wanafunzi wote wanapata umahiri.
Amesema kuna baadhi ya Walimu hawatimizi majukumu yao na wengine wanadiriki kuwaambia wanafunzi baadhi ya masomo ni magumu yakiwemo masomo ya Sayansi na Hisabati ambapo amesema hakuna somo gumu.
Mwakilishi huyo wa Katibu Mkuu TAMISEMI amewataka Wakuu wa Shule na walimu wakuu kuimarisha Ushirikiano na Walimu ili kurahisisha Utendaji kazi na Kuboresha ujifunzaji na ufundishaji.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Maurus Hyera ameahidi kutekeleza maagizo yote ambayo yametolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI.
Baadhi ya walimu wilayani humo wameishukuru serikali kwa kuboresha maslahi ya walimu ikiwemo kuhakikisha walimu ambao hawajapandishwa madaraja wanapandishwa katika mwaka mpya wa fedha wa 2024/2025.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.