Maonesho ya Nane nane 2022 Mkoani Ruvuma imepambwa na Mifugo yenye kushangaza kwa ukubwa wake na kuvutia wananchi.
Akizungumza katika Manesho hayo Mtaalamu wa Mifugo Bahati Luoga amesema Ng’ombe wa Miaka mitatu anakilo 800 na amezaa mara moja.
Mtaalamu amesema Ng’ombe huyo mwenye ukubwa wa uzito wa kilo 800 asili yao ni uholanzi anakula kilo 15 hadi 20 na kunywa maji lita 90 kwa siku.
Luoga amesema ni Ng’ombe hao wanatoa maziwa lita 20 kwa siku na anaumri wa miaka 3.
Ng'ombe huyo hanamadhara yoyote kwa binadamu kwakua ni ng'ombe mpole ,asili yake ni kutoka Uhoranzi anazaa kila mwaka kwa mda miaka nane na kuzeeka.
Luoga ametoa wito kwa kuwakaribisha wanaruvuma na Watanzania wote katika maonesho ya Nane nane ili wakajifunze ufugaji bora.
Imeandaliwa na Janeth Ndunguru
Kutoka kitengo cha Mawasiliano ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Agosti 1,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.