MBEGU bora ya Nguruwe mkubwa wa mwaka mmoja anapatikana katika maonesho ya nane nane Ruvuma.
Hayo amezungumza katika Viwanja vya Nane nane Bwanashamba Francis Chapile kutoka katika Shirika la Karitasi linalopatikana Manispaa ya Songea.
"Nguruwe huyu aina yake ni redwhite amechanganywa na aina nyingine ambayo ni mbegu ya kiwango cha juu (highbred)".
Chapile amesema aina hii ya nguruwe akishazaliwa anakatwa mkia ili madini yanayotoka mkiani yaende kwenye mwili kusababisha mifupa kukomaa kwa haraka .
Amesema ufugaji wa Nguruwe unafaida mara mbili ikiwa kinyesi chake kinatumika kwa kulimia bustani za mboga mboga.
Chapile anawakarisha wananchi wote wapate kujifunza na wajipatie mbegu bora ya vifaranga vya Nguruwe.
Imeandaliwa na Janeth Ndunguru
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Agosti 02 2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.