Na Gustaph Swai-RS Ruvuma
Benki ya NMB imeandaa Semina ambayo imehusisha utoaji wa mafunzo na fursa mbalimbali kwa Walimu wa Kanda ya Kusini yaliyofanyika Katika ukumbi wa Chandamali Uliyopo Mahenge Manispaa ya Songea.
Akizungumza kwenye semina hiyo,Meneja wa NMB Kanda ya Kusini Faraja Raphael amesema,walimu ni wadau wakubwa katika biashara na kwamba wana mchango mkubwa katika Benki ya NMB.
“Tunathamini mchango wao mkubwa kwetu NMB, tumeona tuje na Masuluhisho ambayo yataenda kuwasaidia Walimu, Tunajua wanafanya shughuli mbalimbali nje ya ajira hivyo tumeona tuwawezeshe katika shughuli hizo wanazozifanya na tumeamua kuja na Mwalimu Spesho" amesema Faraja.
Amesisitiza kuwa semina hiyo elekezi imelenga kuboresha ustawi wa watumishi hususani walimu na kuunga Mkono juhudi za Serikali za kuboresha maisha ya watumishi kwa ujumla.
Semina hiyo imeshirikisha walimu kutoka Halmashauri za Manispaa ya Songea na Halmashauri ya Songea ambao wamepewa mafunzo kuhusu elimu ya fedha ,kuweka akiba, mikopo ya elimu,mikopo ya vyombo vya moto, biashara ndogondogo, na mikopo ya kilimo na Bima.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Elizabeth Gumbo akizungumza kwenye mafunzo hayo ameishukuru NMB kwa kuboresha Maisha ya watumishi wakiwemo walimu.
Amesema kongamano hilo lina manufaa makubwa kwa watumishi, ambao wamepewa elimu juu ya Matumizi sahihi ya fedha ,ikiwemo uhifadhi wa fedha na fursa ya mikopo mbalimbali ambayo inaendeshwa na NMB.
Ameongeza kuwa kupitia Kongamano watumishi wamejua sehemu sahihi ya Kwenda kuchukua mikopo ambayo haitowaumiza ni kupitia Benki ya NMB.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.