• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

NMB yatoa msaada wa vifaa katika shule tatu za msingi Songea

Imewekwa kuanzia tarehe: March 12th, 2021

BENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 12 katika shule tatu za msingi zilizopo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

Akikabidhi vifaa hivyo katika shule hizo,Meneja wa NMB Kanda ya Kusini Janeth Shango amezitaja shule zilizopata vifaa hivyo kuwa ni shule ya msingi Legele iliyopata mabati 60 kwa ajili ya kuezeka darasa la kwanza na choo.

Shule nyingine ni Mshanganokati iliyopewa madawati 80 na shule ya msingi Chandamali ambayo imepewa meza 21,viti 21 na kabati nne ambapo amesisitiza kuwa Benki ya NMB imeamua kushirikiana na jamii kwa kutoa msaada katika shule hizo tatu .

“Ingawa Benki ya NMB inapokea maombi mengi,naweza kuahidi kwamba tutaendelea kutoa misaada hii kadri ambavyo tutakuwa tunaweza,tumejipanga kutoa huduma bora kwa jamii’’,alisisitiza Shango.

Kwa upande wake Meneja wa NMB Tawi la Songea David Zake akizungumza kwa nyakati tofauti katika zoezi la utoaji vifaa hivyo,amesema Benki ya NMB ni sikivu kwa sababu imekuwa inarudisha mapato yake ya asilimia moja kwa jamii kila mwaka .

Amesema hali hiyo ndiyo iliyosababisha shule hizo tatu kuwa miongoni mwa shule ambazo zimepata mchango mkubwa kutoka NMB.

Mgeni rasmi katika hafla ya utoaji msaada huo Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Songea Pendo Ndumbaro amesema NMB imemaliza chagamoto ya madawati iliyokuwa inaikabili shule ya msingi Mshanganokati ambayo ilisababisha baadhi ya watoto kukaa chini kwa kukosa madawati.

Amesema NMB imekuwa karibu kwa jamii wilayani Songea kwa kutoa misaada mbalimbali katika shule na vituo vya afya ambapo amesisitiza kwa kazi zinazofanywa na Benki hiyo zinaunga mkono jitihada za serikali kusaidia wananchi.

Naye Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Songea Zakia Fandey amesema msaada huo  utaongeza mahudhurio mazuri ya wanafunzi hasa katika shule msingi Mshanganokati iliyokuwa na uhaba mkubwa wa madawati na kwamba ufundishaji na ujifunzaji utaimarika .

Rehema Milinga ni Mwalimu Mkuu shule ya msingi Mshanganokati  ameishukuru NMB kwa msaada wa  madawati ambapo amesema watoto walikuwa wanaandika chini kwa kuegemea kwenye ukuta ambapo hivi sasa asilimia kubwa ya watoto  wanakaa kwenye madawati.

Nao wanafunzi Mary Haule  na Happy Mbunga kwa niaba ya wanafunzi wenzao wameishukuru NMB kwa msaada wa madawati na mabati vifaa ambavyo wamesema vitawawezesha kusoma kwenye mazingira mazuri.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Machi 12,2021

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.