• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa

Imewekwa kuanzia tarehe: March 15th, 2024

BENKI ya NMB Kanda ya Kusini imetoa msaada wa vifaa vya  ujenzi vyenye thamani ya Zaidi ya shilingi  milioni 29.7 katika shule sita  zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.

Akizungumza kwenye hafla ya ugawaji wa vifaa hivyo iliyofanyika katika shule ya msingi Nangombo mjini Mbambabay, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kusini Faraja Ngingo amevitaja vifaa vilivyotolewa na Benki hiyo kuwa ni mabati na misumari kwa ajili ya kuezekea.

Amezitaja shule zilizonufaika na msaada huo ni  shule tano za  msingi  ambazo ni shule ya Nangombo iliyopata vifaa vyenye thamani ya Zaidi ya shilingi milioni tano,shule ya Chiwindi vifaa vya milioni 4.6,Lundo vifaa vya milioni 4.5,Chinula vifaa vya milioni 4.28,Ndingine vifaa vya milioni 6.9 na sekondari moja ya Ngumbo ambayo imepewa vifaa vya milioni 4.28.

“Vifaa hivi tunavyokabidhi leo ni moja ya ushiriki wetu katika maendeleo ya  jamii,sisi kama Benki tunaowajibu  wa kuhakikisha jamii inayotuzunguka inafaidika kutokana na faida tunayoipata’’,alisisitiza Ngingo.

Amesema kwa miaka kadhaa NMB imekuwa ikisaidia miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi kwa kujikita Zaidi kwenye miradi ya elimu kwa kutoa madawati na vifaa vya kuezekea na sekta ya afya vifaa vya magodoro,vitanda na vifaa vingine vya kusaidia matibabu.

Mgeni rasmi kwenye hafla hiyo Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyasa Salum Ismail ameishukuru Benki ya NMB kwa msaada wa vifaa hivyo ambapo amesema benki hiyo imekuwa inatoa misaada mbalimbali serikalini katika sekta za elimu na afya.

Amesema Benki hiyo pia imekuwa inatoa mchango mkubwa kwenye majanga ambapo katika Wilaya ya Nyasa,NMB imeshiriki kutoa vifaa vya huruma yakiwemo majeneza  kwa watu tisa waliopoteza Maisha hivi karibuni kwa ajali ya gari katika kata ya Lumeme.

Ametoa rai kwa  walimu wa shule ambazo zimekabidhiwa vifaa hivyo vya kuezekea kuhakikisha vinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ambapo pia amewataka wazazi na walezi kuendelea kusimamia maadili na nidhamu ya Watoto   wao tangu wakiwa nyumbani.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Pasifiki Mhapa amesema NMB imekuwa karibu sana na jamii katika kuhakikisha kuwa changamoto za elimu na afya zinapatiwa ufumbuzi.

Hata hivyo amesema mahitaji ya kielimu katika Halmashauri hiyo bado ni makubwa kutokana na idadi ya Watoto wanaokwenda shule kuongezeka hivyo Halmashauri inahitaji wadau kama NMB kusaidia katika maendeleo yaa elimu.

Akizungumza kwa niaba ya walimu wa wakuu waliopata msaada wa vifaa hivyo,Mwalimu Mkuu shule ya msingi  Chinula Mwl.Emanuel Chilwa ameishukuru NMB kwa msaada huo  ambao unakwenda kupunguza changamoto ya vifaa vya ujenzi katika shule hizo.

NMB ni Benki yenye  matawi Zaidi ya 230 nchini,ikiwa na mashine za kutolea fedha (ATM) Zaidi ya 780 nchi nzima,wakala Zaidi ya 20,000 na wateja Zaidi ya milioni sita.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.