SERIKALI kupitia Wizara ya Kilimo imeweka mikakati ya kuwainua vijana kwenye setka ya kilimo ili kuondokana ongezeko la kukosa ajira nchini
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa kilimo, Mheshimiwa Antoy Mavunde, alisema kwenye bajeti ya mwaka huu Wizara imekuja na programu ya “Ijenge kesho iliyobora” lengo ni kuwawezesha vijana kuingia kwenye kilimo.
Mavunde amesema Wizara inaamini vijana wengi nchini wanapenda kilimo lakini kumekuwepo na vikwazo mbalimbali wao kama wizara wamejitahidi kuvitatua kwa kuwatafutia ardhi pamoja na kuwapa mikopo na kuwatafutia masoko ya uhakika ya mazao yao.
“Mpango huo umeanzia na mkoa ya Mbeya na Dodoma ambapo jumla ya hektari elfu 69 zimetengwa kwaajili ya utekelezaji wa program hii kwa Dodoma tumeaanza na Wilaya ya chamwino na Mbeya tumeanza na wilaya ya chunya lengo vijana wajiajiri” alisema Mvunde.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.