Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma imegawa vishikwambi Kwa waheshimiwa madiwani na wakuu wa Idara na Vitengo katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wilaya ya Nyasa.
Mkurugenzi Mtendaji wilaya ya Nyasa Bw.Khalid khalif amesema ni rasmi Wilaya ya Nyasa inaondokana na matumizi ya karatasi katika vikao na hatimaye watatumia teknolojia ya habari na mawasiliano katika vikao na shughuli zote.
Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Kwa matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya nyasa MH.Stewart Nombo amesema Halmashauri ya Nyasa inaendelea kuboresha huduma mbalimbali ili iwe ya Kisasa.
Pichani Ni Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Bw.Khalid Khalif akimkabidhi Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya Kishikwambi, Katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wilaya ya Nyasa mjini Mbambabay
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.