Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma imepokea vifaa Tiba vitakavyotumika kutolea huduma, katika Hospitali ya Wilaya ya Nyasa,vituo vya Afya na zahanati.
Akipokea vifaa Tiba hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Nyasa, Dr.John Mrina amesema kontena la vifaa tiba vimetolewa kwa ufadhili wa Human Bridge wa Nchini Sweden.
Amesema vifaa hivyo vitaboresha huduma bora ya matibabu, kwa Wagonjwa watakaokuja kupata matibabu katika hospitali ya Wilaya na vituo vya Afya na Zahanati.
Hata hivyo amesema baadhi ya Vifaa tiba vilivyopokelewa Vinakwenda kuimarisha huduma bora za afya kwa wananchi wa wilaya ya Nyasa.
Amevitaja baadhi ya vifaa hivyo kuwa ni mashine ya usingizi (Anaesthetic.") ambayo awali kulikuwa na mashine moja na mashine ya kuzuia damu isitoke wakati wa upasuaji hali itakayosaidia kurahisisha utoaji wa huduma ya matibabu kwa Wagonjwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Bw.Khalid Khalif,ameipongeza Serikali ya kwa kuwa na mahusiano mema na nchi za Ulaya ambazo zinatoa msaada wa vifaatiba.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.