Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa imepitisha bajeti ya Tsh bilioni 29.9 kwa mwaka wa fedha 2025/2026 katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya.
Bajeti hiyo imegawanyika katika sekta mbalimbali, ikiwa ni bilioni 17.1 kwa mishahara, bilioni 4.4 kwa matumizi mengineyo, na bilioni 8.3 kwa miradi ya maendeleo.
, Maputo ya ndani yanatarajiwa kufikia bilioni 2.9.
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Mhe. Peres Magiri, aliwasilisha salamu za Serikali na kupongeza juhudi za ukusanyaji wa mapato, akibainisha kuwa yameongezeka kutoka bilioni 1.2 mwaka 2021/2022 hadi bilioni 2.9 mwaka 2025/2026.
Amewataka watumishi wa Halmashauri kuendelea na kasi hiyo ili kuboresha huduma kwa wananchi.
Ametoa tahadhari juu ya tishio la mamba katika maeneo ya maji na kuwaomba wananchi kuwa waangalifu wanapovua au kuoga.
Mbunge wa Jimbo la Nyasa, Mhandisi Stella Manyanya, alisisitiza umuhimu wa wananchi kutumia vituo vya afya vilivyopo ili kuepuka kuchelewa kupata matibabu, hasa kwa wajawazito.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mheshimiwa Starwat Nombo aliwataka madiwani kushirikiana vyema na watumishi wa Serikali katika maeneo yao kwa lengo la kuimarisha ustawi wa jamii.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Bw. Khalid Khalif, aliwataka madiwani kuhamasisha ukusanyaji wa mapato na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu, Bw. Ngonyani, almevitaja vipaumbele vya bajeti hiyo ni kuboresha miundombinu ya elimu, afya, na kuongeza uzalishaji wa mazao ya kimkakati kama kahawa, kokoa, na michikichi, ambapo Tsh milioni 60 zimetengwa kwa ajili ya mbegu za bure
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.