• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

NYAYO inayoaminika kuwa ya Yesu kivutio cha utalii Litembo Mbinga

Imewekwa kuanzia tarehe: May 5th, 2021

KIJIJI cha Litembo kilichopo wilayani Mbinga mkoani Ruvuma kimebarikiwa kuwa na vivutio adimu cha utalii ambavyo huwezi kuviona mahali pengine popote.

Salvius Nyamajabeni ni Mwenyekiti Baraza la Mila na Utamaduni wa kabila la wamatengo katika kijiji hicho aliyechaguliwa tangu mwaka 1958 anasema,Kijiji hicho kina kivutio ambacho kinawashangaza wengi ambacho anakitaja kuwa ni uwepo wa nyayo ya binadamu wa kale ambayo wananchi wa Litembo wanaamini kuwa ni nyayo ya Yesu.

“Kuna alama ya nyayo ya binadamu yenye vidole ambayo imekanyagwa juu ya jiwe miaka mingi iliyopita,sisi wananchi wa Litembo tunaamini kuwa Yesu amekanyaga kwa sababu haifutiki miaka yote’’,anasema Nyamajabeni.

Anasema kila mwaka waumini wa kikristo wanapanda juu kilele cha jiwe la Litembo ambako kuna nyayo na kwenda kuhiji na kwamba eneo hilo pia limewekwa msalaba.

Mwenyekiti huyo anasema kijiji cha Litembo  kina vivutio vingi vya utalii ambavyo havijatangazwa na kufahamika ambapo amelitaja jiwe la Litembo,lina utajiri wa utalii wa kishujaa na kihistoria kutokana na mababu na mabibi zetu takribani 800 waliuwawa na wakoloni wa kijerumani Machi 4,1902,kutokana na kukataa kutawaliwa.

Amelitaja jiwe ambalo yalifanyika mauaji hayo linaitwa Litembo,jina ambalo limetokana na kufanana sana na kichwa cha   mnyama  tembo.

Anasema eneo hilo yalikuwa makazi na maficho ya wazee wakati wa vita dhidi ya wajerumani ambapo ndani ya jiwe hilo kuna pango refu linalotokea katika Kijiji cha Maguu wilayani Mbinga.Inaelezwa ndani ya pango hilo kuna Wanyama wakali,nyoka,maji mengi,pia inadaiwa kuna madini ya zebaki na samani za chuma.

Katibu wa Baraza la Mila na Utamaduni Kata ya Litembo, Bruno Tembo anasema mashujaa hao 800 baada ya kuuawa walizikwa katika makaburi ya Pamoja ya watu 25 katika Kijiji cha Litembo na kwamba ili kuwakumbuka mashujaa hao mnara wa makumbusho  umejengwa kwenye maeneo ya jiwe la Litembo na kwamba kila  mwaka Novemba 28 yanafanyika maadhimisho ya kuwakumbuka wazee 800 waliopambana na wajerumani.

Mwenyekiti Mstaafu wa kijiji cha Litembo Paulo Mwingira anasema serikali ya kijiji hicho kwa kushirikiana na wazee wa mila wa kabila la wamatengo wamejipanga kuhakikisha kuwa vivutio vyote vya utalii wa kihistoria na kishujaa vilivyopo katika eneo hilo vinalindwa na kuendelezwa kwa ajili ya urithi wa kizazi cha sasa na kijacho.

 Afisa Maliasili na Utalii Mkoa wa Ruvuma Afrikanus Challe anasema,wamedhamiria  kuvitangaza vivutio vya utalii wa kihistoria  na kishujaa vilivyopo eneo la Litembo  ili watalii wengi waweze kufika na kuona namna mababu zetu walivyoshiriki katika harakati za ukombozi dhidi ya wakoloni wa kijerumani.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Mei 5,2021

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.