Uchumi wa Mkoa hutegemea Kilimo ambapo zaidi ya asilimia 87 ya wakazi wake hupata riziki yao kupitia sekta ya Kilimo ambayo inachangia pato la Mkoa kwa asilimia 75. Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema Pato la Mkoa wa Ruvuma (Regional/Gross Domestic Product - GDP) limeongezeka kutoka Tshs. 3,680,359,000,000.00 mwaka 2015 hadi Tshs. 5,317,073,000,000.00 mwaka 2019.
Mndeme amesema ongezeko hilo ni sawa na ongezeko la asilimia 44.47 na kwamba pato la Taifa la mtu (Per Capital income) kwa mwaka 2015 lilikuwa Tshs. 2,505,569.00 na limeongezeka hadi Tshs. 3,288,256.00 mwaka 2019 ikiwa ni ongezeko la asilimia 31.23
Mkuu wa Mkoa amesema hayo ni mafanikio makubwa yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli. Mkoa wa Ruvuma una wilaya Tano na Halmashauri nane.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma
Septemba 4,2020
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.