Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma limefanikiwa kukamata vipande 65 vya nyaya za umeme vinavyomilikiwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), ambavyo vilikuwa vimehifadhiwa nyumbani kwa watuhumiwa wawili waliokuwa wakitafuta wateja wa kuviuza.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, SACP Marco Chilya, amesema nyaya hizo zimekamatwa kupitia operesheni maalum inayoendelea kwa ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na taasisi mbalimbali za serikali katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu wa kiuchumi.
Amewataja Watuhumiwa waliokamatwa ni Idrisa Mnimi (21), mkazi wa Matarawe na Ramadhan Kalumbu (19), mkazi wa Mateka, Songea. Wote walikamatwa Aprili 11, 2025 wakiwa na mali hiyo ya serikali.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa TANESCO Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Mashauri Adam, amesema wizi wa miundombinu ya umeme umekuwa changamoto kubwa kwa shirika hilo kwa zaidi ya miaka mitatu, na umesababisha hasara inayokadiriwa kufikia zaidi ya shilingi milioni 150.
Jeshi la Polisi limeahidi kuendelea na operesheni hiyo ili kukomesha kabisa vitendo vya wizi wa miundombinu ya umma mkoani humo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.