Programu ya Uwezeshaji Wananchi kiuchumi inayoitwa Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA) inatarajia kuzinduliwa mjini Songea mkoani Ruvuma Juni 27 mwaka huu.
Uzinduzi huo unatarajia kufanywa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bibi Beng’i Issa kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo kuanzia saa 3 hadi 6 Asubuhi kutakuwa na mkutano wa viongozi wa Mkoa,wakuu wa Wilaya na Makatibu Tawala wa Wilaya,waratibu wa uwezeshaji ngazi ya Mkoa na Halmashauri na viongozi wa majukwaa ya uwekezaji wanawake kiuchumi wa Halmashauri zote,mkutano utafanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Kulingana na ratiba hiyo kuanzia saa 6 mchana hadi saa 10 jioni kutakuwa na mkutano wa wajasiriamali wote Pamoja na viongozi wote,mkutano ambao utafanyika kwenye ukumbi wa parokia ya Bombambili mjini Songea
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.