Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli leo (05.04.2019) amezindua rasmi chuo cha ufundi stadi VETA wilaya ya Namtumbo.
Ujenzi wa chuo hiki umeigharimu serikali shilingi Bilioni 6.32 ambazo zimetolewa na serikali ya Awamu ya Tano.Katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na mamia ya wananchi wa Namtumbo,Rais Magufuli ameonyesha kutofurahishwa na kiasi kikubwa cha fedha kilichotumika kujenga mradi huu na kuadiza wizara kufanya uchunguzi wa matumizi sahihi ya fedha hizo.
Chuo cha VETA Nantumbo kitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 350 wa muda mrefu na wanafunzi 600 wa muda mfupi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.