Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imeendelea kuimarishaji miundombinu katika Mkoa wa Ruvuma
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed ameitaja baadhi ya miundombinu hiyo kuwa ni Pamoja na upanuzi na ukarabati wa Kiwanja cha Ndege Songea kimekarabatiwa kwa gharama ya shilingi bilioni 37.
Miundombinu mingine ameitaja kuwa ni ujenzi wa soko katika kijiji cha Peramiho wilayani Songea unaendelea kwa gharama ya Zaidi ya shilingi milioni 200.7 na ujenzi wa kituo cha mabasi katika kijiji cha Parangu unaendelea kwa gharama ya Zaidi ya shilingi miliobi 225.
Kulingana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Serikali pia imejenga Bandari kubwa na ya kisasa ya Ndumbi katika ziwa Nyasa kwa gharama ya bilioni 12.5 .
Amebainisha kuwa Bandari hiyo ina gati lenye urefu mita 160 kwenda ziwani, urefu (jetty head) wa mita 20.4, ramp urefu wa kwenda Ziwani mita 40 urefu (Ramp head) mita 10, ghala la kuhidhi mizigo inayoathiriwa na mvua lenye mita za ukubwa 2,020, eneo lenye sakafu ngumu (heavy heavy yard) kwa ajili kuhifadhi mizigo isiyoathiriwa na mvua lenye ukubwa wa meta za mraba 9,030 na jengo la kupumzikia abiria na ofisi na nyumba za watumishi.
Amesema serikali pia inatarajia kujenga Bandari mpya ya kisasa ya Mbamba Bay kwa lengo la kuimarisha Ushoroba wa Maendeleo wa Mtwara (Mtwara Development Corridor), ambayo ni njia fupi na rahisi ya kuhudumia mzigo wa Malawi kutokea Bandari ya Mtwara.
Amesema bandari hiyo inaunganishwa kwa barabara hadi Bandari ya Mbamba Bay na kuunganisha hadi Bandari za Malawi kupitia majini.
Hata hivyo amesema Ili kutekeleza mradi huo mkubwa, Serikali ya Awamu ya sita imetoa Zaidi ya shilingi bilioni 70 kwa ajili ya ujenzi wa Bandari kubwa na kisasa ya Mbamba Bay.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.