WAKAZI wa kijiji cha Ndonga kata ya Liwundi Halmashauri ya wilaya Nyasa mkoani Ruvuma,wameishukuru serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kujenga barabara mpya yenye urefu wa kilometa saba inayounganisha kijiji hicho na Njambe ambayo imesaidia kuondoa kero za muda mrefu zilizosababishwa na kukosekana kwa barabara ya uhakika.
Barabara hiyo inajengwa na Wakala wa Barabara za mjini na vijijini(Tarura) kwa gharama ya zaidi ya Sh.milioni 220, ambapo itaharakisha shughuli za uchumi na uzalishaji mali hasa kusafirisha dagaa kutoka ziwa nyasa kwenda maeneo mengine ya Tanzania.
Marietha Mkondola alisema, katika kijiji hicho hakukuwa na huduma yoyote ya mawasiliano ya barabara tangu uhuru mwaka 1961,badala yake wananchi walipotaka kusafiri kwenda maeneo mengine wakiwamo watumishi wa umma walilazimika kutumia mitumbwi na boti hali ambayo imechelewesha sana uchumi wao.
Aidan Mbele alisema,tangu serikali ya awamu ya sita ilipoingia madarakani,wameshuhudia maendeleo makubwa katika kijiji chao ambapo serikali imejenga na kuboresha huduma za kijamii ikiwamo umeme na barabara.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.