Moja ya mafanikio makubwa ya serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ni kumaliza kero ya miaka mingi ya wananchi wa Wilaya za Nyasa mkoani Ruvuma na Ludewa mkoani Njombe baada ya kukamilisha ujenzi wa daraja la Ruhuhu kwa asilimia 100.
Daraja la Ruhuhu lililopo katika Mto Ruhuhu unaomwaga maji yake ziwa Nyasa, lina urefu wa mita 98.01 linaunganisha Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma na Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe. Ujenzi wa daraja hilo ulikamilika tarehe 15 Oktoba 2021 kwa gharama ya Tsh. 8.976 bilioni.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.