MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa mabilioni ya fedha kutekeleza miradi ya maji Wilayani Nyasa.
Ameitaja miongoni mwa miradi inayotekelezwa kuwa ni mradi wa maji Kilosa Mbambabay unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni nne,Mradi wa maji Liuli bilioni 4.7,mradi wa maji Mwelampya Lituhi shilingi bilioni 6.4 na mradi wa maji Ngumbo shilingi bilioni 2.5
“Wilaya ya Nyasa katika Mkoa wa Ruvuma ndiyo yenye miradi mingi mikubwa ya maji ambayo ikikamilika inakwenda kumaliza changamoto ya maji katika kata zote “,alisema Kanali Thomas.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.