Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amekagua miradi mitatu ya maji yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 3.5 fedha zilizotolewa na Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Miradi aliyoikagua ni mradi wa maji kata ya Amanimakoro uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 774 ambao tayari unawahudumia wananchi,mradi wa maji Kata ya Mbangamao unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.8 na mradi wa maji Ruvuma chini Kata ya Mpepai unaogharimu shilingi bilioni 1.3.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi katika kata hizo wamemshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwatua ndoo kichwani baada ya kumaliza kero ya maji ya muda mrefu.
Akizungumza kwa nyakati tofauti baada ya kukagua miradi hiyo,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ameagiza kuhakikisha vyanzo vya maji vinalindwa ili miradi iwe endelevu..
Serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni 42 kutekeleza miradi 35 ya maji katika Wilaya zote tano mkoani Ruvuma.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.