RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemteua Brigedia Jenerali Wilbert Augustine Ibuge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,ambaye anachukua nafasi ya Christina Mndeme ambaye amekuwa Naibu Katibu Mkuu CCM Tanzania Bara.Kabla ya uteuzi huo Balozi Ibuge alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kwa mujibu wa Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,Wakuu wa Mikoa wote walioteuliwa pamoja na wakuu wa Taasisi wanatarajiwa kuapishwa Mei 18 mwaka huu Ikulu jijini Dar es salaam.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.