Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amekagua miradi mikubwa miwili ya maji yenye thamani ya shilingi bilioni 11 katika Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.
Miradi hiyo inatekelezwa katika kata za Lituhi na Liuli ambapo jumla ya vijiji 11 katika kata hizo zitanufaika.
Kati ya fedha hizo kata ya Lituhi imetengewa shilingi bilioni 6.5 na Kata ya Liuli imetengewa shilingi bilioni 4.7
Miradi yote miwili inatarajia kukamilika Aprili 2023 .Kukamilika kwa miradi hii kutatua changamoto ya maji ambayo imekuwa kero kwa miaka mingi kwa wananchi wa mwambao mwa ziwa Nyasa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.