• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RAIS Samia apongeza mradi wa ujenzi wa uwanja wa ndege Songea

Imewekwa kuanzia tarehe: September 23rd, 2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akisikiliza taarifa kutoka kwa Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa kuhusu ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Songea mara baada ya kuwasili Mkoani Ruvuma 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekagua na kupokea taarifa ya ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Songea ambao umekamilika kwa asilimia 100 Mkoani Ruvuma.

Rais Dkt. Samia amekagua Kiwanja hicho, leo Septemba 23, 2024 mara baada ya kuwasili Mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo, kuweka mawe ya msingi ya miradi na kuzungumza na wananchi.

Rais Dkt. Samia amepokea taarifa ya ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Songea uliohusisha upanuzi na kuongeza urefu wa barabara ya kuruka na kutua Ndege, ujenzi maegesho mapya ya Ndege (Apron), ujenzi wa barabara moja ya kiungio, ujenzi wa mnara wa waongoza ndege (Control Tower), kuimarisha maeneo ya usalama kiwanjani pamoja na Ununuzi, usimikaji wa taa za kuongozea ndege na gari la zimamoto.

Akitoa taarifa mbele ya Rais, Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa ameeleza kuwa Serikali ilitoa kiasi cha Shilingi Bilioni 40.87 kukarabati na upanuzi Kiwanja cha Ndege cha Songea ambao hivi sasa utekelezaji wake umekamilika kwa asilimia 100. 

Bashungwa ameeleza kuwa kukamilika kwa ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Songea umerahisisha huduma za usafiri na usafirishaji kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kutoka ndani na nje ya nchi ambapo hivi sasa ndege za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) zinatua mara 3 kwa wiki.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara (TANROADS) Mhandisi Mohamed Besta ameeleza kuwa kazi zilizofanyika za uboreshaji wa Kiwanja cha Ndege cha Songea ni pamoja na ujenzi wa barabara ya kuruka na kutua ndege (runway) kutoka mita 1,625 na upana wa 23 hadi kufikia mita 1,860 na upana wa mita 30 pamoja na ujenzi wa maegesho ya ndege (Apron) unaoruhusu ndege nne (4) aina ya Q400  Bombadier pamoja na ndege ndogo tatu (3) kupaki kwa wakati mmoja na hivyo kufanya Kiwanja hicho kufikia Kiwango cha 3C kwa mujibu wa viwango vya ICAO.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Abdul Mombokaleo ameeleza kuwa baada ya kukamilika kwa uboreshaji wa Kiwanja cha Ndege cha Songea matarajio ni idadi ya abiria kuongezeka ambapo takwimu zimeoneshwa toka mwaka 2021 abiria walikuwa 3,900 na sasa wamefikia abiria 19,620.

Mradi wa Ukarabati na Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Songea ni utekelezaji wa mikakati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kuongeza ufanisi katika sekta ya usafiri na usafirishaji ili kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.