Mabadiliko madogo kwenye Baraza la Mawaziri kama yalivyotangazwa leo na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan. Ofisi ya Rais TAMISEMI – Waziri atakuwa ni Ummy Mwalimu na Manaibu watabaki kama walivyokuwa. Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora – Waziri atakuwa Mohamed Mchengerwa. Ofisi ya Rais Kazi Maalum – Kept. George Mkuchika. Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira – Waziri atakuwa ni Seleman Jafo na naibu wake atakuwa Hamadi Hassan Chande. Ofisi ya Waziri Mkuu Sera – Waziri ataendelea kuwa Jenista Mhagama. Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji – Waziri atakuwa Geofrey Mwambe na Naibu Waziri atakuwa ni William Ole Nasha. Wizara ya Fedha na Mipango – Waziri atakuwa Mwigulu Nchemba na Naibu wake atakuwa Hamad Masauni. Wizara ya Katiba na Sheria – Waziri atakuwa Prof. Palamagamba Kabudi na naibu wake atakuwa Geofrey Mizengo Pinda. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki – Waziri atakuwa ni Balozi Liberata Mulamula (Pichani), na naibu wake atakuwa Mbarouk Nassor Mbarouk. Wizara ya Viwanda na Biashara – Waziri atakuwa ni Prof. Kitila Mkumbo na naibu wake atakuwa Exaud Kigae Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo – Waziri atabaki yuleyule Innocent Bashingwa lakini naibu wake atakuwa Pauline Gekul. Wizara ya Afya – Waziri atabaki kuwa Dkt. Dorothy Gwajima lakini atakuwa na manaibu wawili ambao ni Dkt. Godwin Mollel na Mwanaidi Ally Khamis.Wizara wa Mifugo na Uvuvi – Waziri atabaki kuwa Mshinda Ndaki lakini naibu wake atakuwa ni Abdallah Ulega. Wizara ambazo hazijaguswa zitaendelea kubaki kama zilivyo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.