SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imeweza kutoa ajira mbalimbali zaidi ya 47,374.
Hayo yamesemwa na Mbunge wa Viti Maalum na Mwakilishi wa Wafanyakazi Bungeni Tanzania Bara Dkt.Alice Kaijage wakati anazungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Songea mjini Peramiho mkoani Ruvuma.
Dkt. Kaijage amesisitiza kuwa Rais Samia ataendelea kutoa nafasi za ajira kwa Watanzani ambapo kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 Serikali imetenga ajira 27,000 katika nafasi mbalimbali.
“Katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali ilitenga bajeti kwa ajili ya kuwapindisha vyeo watumishi 12,000, na pia imeweza kuwabadilisha Kada (Muundo) watumishi mbalimbali na kiasi cha Shilingi Bilioni 2.5 zimetumika’’,alisema.
Mheshimiwa Dkt. Kaijage katika ziara yake ameweza kusikiliza kero mbalimbali za watumishi ambapo ameahidi kuzifanyia kazi atakapofika bungeni Dodoma.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.