KATIKA kipindi cha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Mkoa wa Ruvuma umepokea Jumla ya shilingi Bilioni 249.7 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema kati ya fedha zilizopokelewa,fedha za ndani shilingi Bilioni 128 na Fedha za nje shiling bilioni 121.7 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo miradi ya sekta za elimu,afya,,barabara ,Viwanja vya ndege,bandari,Maji,umeme,kilimo,uvuvi,viwanda,utalii,mifugo na Uwezeshaji wananchi kiuchumi
Mkoa wa Ruvuma una ukubwa wa kilomita za mraba 63,669, Wilaya Tano,Halmashauri Nane na idadi ya Wakazi wapatao 1,848,794 kwa mujibu wa sensa ya watu ya mwaka 2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.