Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa shilingi bilioni nne katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma kwa lengo kutekeleza miradi ya afya.
Hayo yamesemwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Mheshimiwa Michael Mbano alipofanya ziara ya siku tatuya kutembelea miradi ya afya inayoendelea kujengwa katika kata za Tanga, Lilambo na kata ya Mletele.
Mheshimiwa Mbano amebainisha kuwa kati ya fedha hizo kituo cha afya Mletele kimegharimu shilingi milioni 845, kituo cha afya Lilambo shilingi milioni. 550 na Kituo cha afya Mletele kimejengwa kwa shilingi milioni 545.
Hata hivyo amesema serikali imetoa kiasi cha shilingi bilioni moja kutekeleza mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Manispaa ya Songea katika Mtaa wa Sanangula
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.